Uhaba mkubwa wa mvua ambao haujawahi kutokea mkoani Dodoma utaathiri vibaya mavuno ya alizeti mwaka huu. Dodoma ni mkoa wa pili kwa mavuno mengi ya zao la alizeti baada ya Singida na ni mkoa wenye viwanda vingi vidogo na vya kati vya kusindika mafuta ya alizeti. Wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Chamwino zimekumbwa na upungufu mkubwa wa mvua. Wasindikaji wa mafuta haya mkoani hapa wana wasi wasi mkubwa kwa upatikanaji wa kutosha wa mbegu za alizeti kwa ajili ya usindikaji kwa mwaka huu. Selina Kuziganika wa SEEKU Oil Mills ya hapa Dodoma na ambaye ni mweka hazina wa chama cha wasindika mafuta mkoani hapa CEZOSOPA,anasema; " Kwa kweli mwaka huu, kuna wasi wasi wa baadhi ya viwanda kufungwa kabisa na bei ya mbegu ya alizeti kupanda sana."
Wadau wa alizeti wa Morogoro, Singida, Chunya, Ileje, Tabora na Shinyanga vipi hali ya zao huko? Kama hali itaendelea kuwa hivi je uwezo wa kujaza lile soko la mafuta utakuwaje. Wataalam wanashauri nini juu ya kilimo cha umwagiliaji?
No comments:
Post a Comment