Uhaba mkubwa wa mvua ambao haujawahi kutokea mkoani Dodoma utaathiri vibaya mavuno ya alizeti mwaka huu. Dodoma ni mkoa wa pili kwa mavuno mengi ya zao la alizeti baada ya Singida na ni mkoa wenye viwanda vingi vidogo na vya kati vya kusindika mafuta ya alizeti. Wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Chamwino zimekumbwa na upungufu mkubwa wa mvua. Wasindikaji wa mafuta haya mkoani hapa wana wasi wasi mkubwa kwa upatikanaji wa kutosha wa mbegu za alizeti kwa ajili ya usindikaji kwa mwaka huu. Selina Kuziganika wa SEEKU Oil Mills ya hapa Dodoma na ambaye ni mweka hazina wa chama cha wasindika mafuta mkoani hapa CEZOSOPA,anasema; " Kwa kweli mwaka huu, kuna wasi wasi wa baadhi ya viwanda kufungwa kabisa na bei ya mbegu ya alizeti kupanda sana."
Wadau wa alizeti wa Morogoro, Singida, Chunya, Ileje, Tabora na Shinyanga vipi hali ya zao huko? Kama hali itaendelea kuwa hivi je uwezo wa kujaza lile soko la mafuta utakuwaje. Wataalam wanashauri nini juu ya kilimo cha umwagiliaji?
Karibu kwenye blog hii ya ulimwengu wa Alizeti. Blog hii inahusu taarifa mbalimbali za zao la Alizeti pamoja na maendeleo yake na mnyororo wa thamani wa bidhaa zake, ndani na nje ya nchi. Taarifa na taaluma mbalimbali za Kilimo na usindikaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na mbegu za Alizeti zitawekwa hapa kwa ajili ya kuwanufaisha wadau wa zao hili. Tafadhali, furahia ulimwengu wetu na kama una taarifa yoyote ya kuchangia, unakaribishwa sana.
Thursday, May 2, 2013
ASA MBIONI KUTOA MBEGU MPYA YA ALIZETI (BOFYA KUTOA MAONI)
Ni taarifa njema kutoka kwa wakala
wa mbegu wa serikali (ASA) kuwa iko mbioni kutangaza mbegu mpya ya alizeti
iliyogunduliwa juzi na moja ya vituo vyake vya utafiti. Akitoa taarifa hizo
katika mkutano wa shirika la maendeleo lisilo la kiserikali la RLDC katika
mkutano na washirika uliofanyika mkoani Singida wiki iliyopita, Mkurugenzi wa
Masoko wa ASA Mr. Kawamala alisema mbegu hiyo inauwezo mkubwa kuliko Record
ambayo kwa sasa ndiyo inayoongoza nchini. Mbegu hiyo vile vile inauwezo mkubwa
wa kuvumilia ukame. Bado chanzo chetu kinatafuta taarifa zaidi juu ya mbegu hii
na itawajuza wadau pindi taarifa hizo zitakapotufikia. Kama mdau una taarifa
yoyote karibu utujuze.
Subscribe to:
Posts (Atom)