Pages

Thursday, May 2, 2013

UHABA WA MVUA KUDHURU MAVUNO YA ALIZETI DODOMA ( CLICK TO COMMENT)

Uhaba mkubwa wa mvua ambao haujawahi kutokea mkoani Dodoma utaathiri vibaya mavuno ya alizeti mwaka huu. Dodoma ni mkoa wa pili kwa mavuno mengi ya zao la alizeti baada ya Singida na ni mkoa wenye viwanda vingi vidogo na vya kati vya kusindika mafuta ya alizeti. Wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Chamwino zimekumbwa na upungufu mkubwa wa mvua. Wasindikaji wa mafuta haya mkoani hapa wana wasi wasi mkubwa kwa upatikanaji wa kutosha wa mbegu za alizeti kwa ajili ya usindikaji kwa mwaka huu. Selina Kuziganika wa SEEKU Oil Mills ya hapa Dodoma na ambaye ni mweka hazina wa chama cha wasindika mafuta mkoani hapa CEZOSOPA,anasema; " Kwa kweli mwaka huu, kuna wasi wasi wa baadhi ya viwanda kufungwa kabisa na bei ya mbegu ya alizeti kupanda sana."
Wadau wa alizeti wa Morogoro, Singida, Chunya, Ileje, Tabora na Shinyanga vipi hali ya zao huko? Kama hali itaendelea kuwa hivi je uwezo wa kujaza lile soko la mafuta utakuwaje. Wataalam wanashauri nini juu ya kilimo cha umwagiliaji?

ASA MBIONI KUTOA MBEGU MPYA YA ALIZETI (BOFYA KUTOA MAONI)

 


Ni taarifa njema kutoka kwa wakala wa mbegu wa serikali (ASA) kuwa iko mbioni kutangaza mbegu mpya ya alizeti iliyogunduliwa juzi na moja ya vituo vyake vya utafiti. Akitoa taarifa hizo katika mkutano wa shirika la maendeleo lisilo la kiserikali la RLDC katika mkutano na washirika uliofanyika mkoani Singida wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Masoko wa ASA Mr. Kawamala alisema mbegu hiyo inauwezo mkubwa kuliko Record ambayo kwa sasa ndiyo inayoongoza nchini. Mbegu hiyo vile vile inauwezo mkubwa wa kuvumilia ukame. Bado chanzo chetu kinatafuta taarifa zaidi juu ya mbegu hii na itawajuza wadau pindi taarifa hizo zitakapotufikia. Kama mdau una taarifa yoyote karibu utujuze.